


Hali ilivyokuwa siku ya mwisho uboreshaji daftari la mpigakura Dar
Dar es Salaam. Wakati leo Machi 25, 2025 ikiwa ni siku ya mwisho ya uboreshaji wa daftari la mpigakura kwa Mkoa wa Dar es Salaam, baadhi ya wananchi wamesema hawakupata taarifa ya uongezwaji wa siku mbili, pia shughuli zao za kila siku ndiyo zimewafanya kwenda vituoni kwa wingi hasa muda wa jioni. Hata hivyo, wamepongeza…

MCT yatimiza miaka 30 ikiwatambua Nyerere, Mwinyi kuhimiza uhuru wa habari
Arusha. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Philip Mpango amesema kumekua na mabadiliko ya sheria, sera na utashi wa kisiasa kuviwezesha vyombo vya habari kutekeleza majukumu yao kikamilifu. Amesema hayo leo Jumanne Julai 15, 2025 wakati akifungua kongamano la pili la mabaraza ya Habari barani Afrika (Nimca) iliyofanyika jijini hapa kuwa…

ACT Wazalendo: Tuna majawabu changamoto za korosho
Tandahimba. Chama cha ACT-Wazalendo, kimedai kina majawabu ya changamoto zinazowakumba wakulima wa zao korosho nchini, ikiwemo bei ndogo na makato wanayokatwa wakati wa kuziuza. Kimejinasibu kuwa majibu ya changamoto ikiwemo upatikanaji wa mbolea na soko la uhakika la zao hilo, yanayotokana na ACT Wazalendo kuwa na sera na muundo mzuri wa kuwatumikia wakulima. Hayo yalielezwa…

Mahakama yamuonya Malisa kutofika mahakamani
Dar es Salaam: Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu imemuonya mwanaharakati Godlisten Malisa, ambaye anashiriki katika kesi ya jinai pamoja na meya mstaafu, Boniface Jacob, maarufu Boni Yai. Mahakama hiyo imesema kwamba, endapo Malisa hatohudhuria usikilizwaji wa kesi yao siku nyingine, atachukuliwa hatua ikiwamo kupelekewa mahabusu. Katika kesi hiyo, wawili hao wanakabiliwa na mashitaka matatu ya…

Wakili Mwasipu: Lissu anatuhumiwa kuhamasisha vurugu maandamano ya Chadema
Dar es Salaam. Wakili wa Chadema, Hekima Mwasipu amesema Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara, Tundu Lissu anashikiliwa kituo cha Polisi Mbweni, Dar es Salaam akituhumiwa kuhamasisha watu kufanya vurugu kupitia maandamano yaliyoitishwa na chama hicho. Lissu ni miongoni mwa viongozi na wanachama zaidi ya 40 wa chama hicho, akiwamo mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, waliokamatwa kwa nyakati…

Vita katika sanduku la kura CCM, majimbo haya hapatoshi
Dar es Salaam. Kinyang’anyiro cha kuisaka tiketi ya kugombea ubunge wa majimbo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), kimefikia katika sanduku la kura za maoni, huku mchuano mkali ukitarajiwa Makambako, Iringa Mjini, Kibamba, Namtumbo na Kinondoni. Majimbo hayo ni machache kati ya mengi yanayotarajiwa kuwa na mchuano mkali wa kura za maoni, kutokana na kile kinachoelezwa…

YALIYOJIRI KWENYE MAGAZETI LEO JUMATATU JULAI 8, 2024
Hello! habari ya wasaa huu, karibu uweze kupitia habari kemkem kutoka nyanja tofauti zilizopewa kipaumbele katika kurasa za magazeti ya leo Jumatatu Julai 8, 2024 kutokea Jijini Dar es Salaam, Tanzania. #koncepttvupdates

Watoto wanaotumikishwa Zanzibar kutoka Bara waanza kusakwa
Unguja. Katika kukabiliana na tatizo la usafirishaji wa watoto kutoka Bara kwenda Zanzibar kwa ajili ya ajira za utotoni, Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama imeanza kufanya ukaguzi kwenye meli zinapowasili katika Bandari ya Malindi ili kubaini uwapo wa watoto hao. Katika operesheni iliyofanyika kwa siku nne kuanzia Aprili 18 hadi 21…

WATU WATATU WATEKETEA KWA MOTO BAADA YA MALORI KUGONGANA USO KWA USO NA KUWAKA MOTO
Farida Mangube, Morogoro WATU watatu wamefariki Dunia mkoani Morogoro kutokana na ajali ya magari mawili ya mizigo kugongana na kuteketea kwa moto. Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Alex Mkama amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Machi 04, 2025 katika eneo la Nanenane barabara kuu ya Morogoro – Dar es Salaam, kata ya Tungi,…