
Riba inavyotafuna mabilioni miradi ya maendeleo
Dar es Salaam. Ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayosimamiwa na taasisi za umma umeendelea kuwagharimu walipakodi, kutokana na riba inayotozwa Serikali na wakandarasi wa miradi hiyo. Hiyo ni kwa mujibu wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, katika ripoti yake ya mwaka unaoishia Machi 2023 iliyowasilishwa bungeni jana…