Waombolezaji watoa heshima za mwisho – DW – 21.05.2024

Raia hao mamia kwa maelfu waliobeba bendera za taifa hilo na picha za Ebrahim Raisi wameshuhudiwa katika uwanja wa Central square mjini Tabriz wakitembea kando ya gari lililobeba majeneza ya Raisi na maafisa wengine saba. Mji huo ndiko alikokuwa akielekea kiongozi huyo na ujumbe wake wakati helikopta waliyokuwa wakisafiria ilipopata ajali Jumapili. Mwili wa Raisi…

Read More

Viwanja vipya vya Afcon kukamilika mwakani

Dodoma. Serikali imesema ujenzi wa viwanja vipya vya michezo kwa ajili ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027), unatarajiwa kukamilika mwakani ili kupisha ukaguzi wa kikanuni. Tanzania, Kenya na Uganda zitaandaa fainali za Kombe la Mataifa Afrika mwaka 2027 ikiwa ni mara ya kwanza nchi hizo zinafanya hivyo. Hayo yamesemwa leo na…

Read More

Safari ya Serikali kuhamia Dodoma kukamilika mwakani

Dodoma. Safari ya Serikali kuhamia jijini hapa  itakamilika  baada ya mpango kazi maalumu na ujenzi wa awamu ya pili wa majengo ya ofisi za wizara na taasisi utakapohitimishwa mwaka 2025. Aidha, Serikali imesema hadi sasa watumishi wa umma 25,039 wameshahamia huku taasisi zilizohamia zikiwa ni 65.Naibu Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge,…

Read More

Tabora, Ihefu mechi ya matumaini

LEO Jumatano katika Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora kutapigwa mechi ya kibabe kati ya wenyeji Tabora United na Ihefu ambayo imebeba matumaini makubwa ya timu hizo mbili kwa msimu huu. Mchezo huo ni wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa 28 kwa kila timu na matokeo yoyote yatakayopatikana yatabadili mambo mengi hususan kwenye nafasi ambazo…

Read More

Frateri wa Kanisa Katoliki Tanga adaiwa kujinyonga

Lushoto. Frateri wa Kanisa Katoliki Shirika la Roho Mtakatifu Jimboni Tanga, Rogassion Hugho, anadaiwa kujinyonga hadi kufa. Hili ni tukio la pili  kwa viongozi wa dini kudaiwa kujinyonga. Mei 16, 2024 mkoani Dodoma, Askofu Mkuu wa Makanisa ya Methodist, Joseph Bundala naye alidaiwa kujinyonga ndani ya ofisi yake iliyopo katika kanisa hilo eneo la Meriwa…

Read More

Dodoma Jiji, Yanga vita iko hapa, Arajiga kati

KWA mashabiki wa Dodoma Jiji wanajiuliza kwanini timu hiyo kwanini haijafunga bao katika mechi nne mfululizo za Ligi Kuu Bara zilizopita wakati kesho itakapoikaribisha Yanga saa 10:00 jioni, Uwanja wa Jamhuri Dodoma. Swali hilo linatokana na safu butu ya ushambuliaji inayoikumba timu hiyo ambapo katika michezo minne imeshindwa kabisa kufunga bao lolote tangu mara yake…

Read More

Serikali yaeleza inachofanya kupambana na kichaa cha mbwa

Dodoma. Serikali ikishauri wadau kutoa chanjo ya kichaa cha mbwa kupitia sekta binafsi, imetaja mikoa inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanyama hao. Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti ametoa ushauri huo bungeni leo Mei 21, 2024 alipojibu maswali ya mbunge wa Viti Maalumu, Yustina Rahhi. Katika swali la nyongeza, mbunge huyo…

Read More

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Serikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali kuu, Bunge, mahakama, vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na taasisi 65 wameshahamia Dodoma na wanaendelea kutekeleza majukumu yao wakiwa makao makuu ya nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Hatua hiyo imekuja baada ya zoezi la kuhamisha makao makuu ya Serikali kutoka Dar es Salaam…

Read More