
Siri ya Taliss ubingwa wa kuogelea hii hapa
Nahodha wa Taliss Swim Club, Delbert Ipilinga amefichua siri ya kuibuka washindi wa jumla kwenye michuano ya 16 ya Klabu Bingwa Tanzania (TNCC) kuwa ni bidii na uthubutu. Klabu hiyo ilikusanya pointi 385 katika michuano ya siku mbili iliyofanyika katika Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. “Nashukuru tumetwaa…