
Iringa kutumia Sh4.4 bilioni utekelezaji miradi ya maendeleo
Iringa. Halmashauri ya Manispaa ya Iringa inatumia zaidi ya Sh4.4 bilioni kutekeleza miradi ya maendeleo. Imeelezwa kati ya fedha hizo, Sh2.6 bilioni zinaboresha miundombinu ya jengo la kitega uchumi linalojengwa eneo la stendi ya zamani, ambako pia kunajengwa jengo la ghorofa mbili litakalotumiwa na wafanyabiashara. Hayo yamebainishwa leo Ijumaa Mei 17, 2024 wakati wa ziara…