
NYUMA YA PAZIA: Mbappe na karatasi zake za ushahidi, kuna maswali?
“..USHAHIDI upi mwingine unahitaji?” Hakusema mdomoni. Moyo wake ulikuwa unaongea. Asingeweza kutamka hivyo mdomoni wakati akirekodi video yake ya kuaga. Kylian Mbappe. Amewaaga PSG mapema wiki hii. Anaondoka zake PSG. Lilikuwa suala la muda tu. Alionekana mtulivu wakati akiaga. Mara ya mwisho serikali ya Ufaransa iliingilia kati kuondoka kwake. Alipoamua kubaki ikawa sherehe kwa Wafaransa….