Mfungwa atoa ushahidi kortini jinsi Mkuu wa Gereza alivyochukua Sh45 milioni
Dar es Salam. Mfungwa anayetumikia kifungo cha miaka 20 gerezani kwa kukutwa na meno ya tembo, Song Lee, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jinsi aliyekuwa Mkuu wa Gereza la Ukonga, Josephat Mkama alivyopokea Sh45 milioni ili amtoe gerezani na kumwachia huru. Raia wa China Song ni mfungwa namba 585/2019 katika Gereza la Segerea. Mahakama…