
RC MANYARA AAGIZA SOKO JIPYA KATESH LIANZE KUTUMIKA.
Na John Walter -Hanang’ Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga ameiagiza Halmashauri ya wilaya ya Hanang’ kukamilisha haraka taratibu zote ili soko jipya lianze kutumiwa na wafanyabiashara. Aidha,ameagiza shughuli katika soko hilo kuanza mara moja kabla ya siku ya Ijumaa Mei 24, 2024 ili kutoa huduma kwa Wananchi na kuchochea uchumi wa wafanyabiashara, Halmashauri…