
ACT yaomboleza msiba wa Abass Mwinyi, yasitisha kampeni
Unguja. Chama cha ACT-Wazalendo kimesitisha mkutano wa hadhara na ratiba zingine za kampeni zilizopangwa kufanyika leo Alhamisi Septemba 25, 2025 ili kuomboleza msiba wa Abass Ali Mwinyi. Abass ambaye ni kaka mkubwa wa Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi amefariki dunia leo Septemba 25 katika hospitali ya Lumumba mjini Unguja na anatarajiwa kuzikwa kesho…