
Aliyeshtakiwa kwa kula, kulala Hoteli ya Serena bila kulipa afutiwa kesi
Dar es Salaam. Mahakama ya Mwanzo Kariakoo imemfutia kesi na kumwachia huru mfanyabiashara aliyeshtakiwa kwa kujipatia huduma ya chakula na malazi katika Hoteli ya Serena kwa njia ya udanganyifu. Mshtakiwa Denis Mfumbulwa (44) alidaiwa kujipatia huduma hizo zenye thamani ya Sh21.4 milioni bila kulipa, akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria. Mfumbulwa amefutiwa kesi Mahakama ikieleza…