
AKILI ZA KIJIWENI: Kijiwe kimembariki Yondani Pamba
IWE ni umri sahihi au sio sahihi, wote tunakubaliana kwamba Kelvin Yondani ‘Vidic’ ni mtu mzima hasa kwenye Ligi yetu ya Tanzania Bara ukilinganisha na mabeki wengi wa kati. Nyaraka zake mbalimbali zinaonyesha kuwa alizaliwa Oktoba 4, 1984 hivyo kwa sasa tayari ametimiza miaka 40 hivyo kiuhalisia wachezaji wengi wa Ligi Kuu ni wadogo zake…