
Watoto 122 waokolewa wakitumikishwa kwenye madanguro, kuombaomba
Dodoma. Jeshi la Polisi limewaokoa watoto 122 waliokuwa wakitumikishwa katika biashara ya ukahaba kwenye madanguro, kuomba mitaani, na kwenye makazi ya watu. Watoto hao wameokolewa katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024. Hayo yamesemwa bungeni leo Mei 15, 2024 na Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Yusuf Masauni alipowasilisha bungeni makadirio ya mapato na…