
Mahamat Deby anavyobeba mustakabali wa Chad
Kishindo cha Mei 10, mwaka huu kimewaacha wananchi wa Chad midomo wazi baada ya kutangazwa kwa Mahamat Idriss Deby Itno, maarufu kama Mahamat Kaka kuwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika mapema mwezi huu. Matokeo ya uchaguzi huo yalitarajiwa kutangazwa Mei 21, hata hivyo yametangazwa mapema kuliko ilivyotarajiwa, jambo ambalo limeibua maswali na kuwafanya wananchi kuingia barabarani…