
NSSF YASHIRIKI MKUTANO MKUU WA ATE, YAZUNGUMZIA MSAMAHA WA TOZO NA MATUMIZI YA TEHAMA
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umeshiriki mkutano mkuu wa 65 wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE). Mkutano huo ulifunguliwa tarehe 20 Juni 2024 na Mhe. Patrobas Katambi, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ambaye alimuwakilisha Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Deogratius Ndejembi. Akizungumza katika mkutano huo,…