
Mgogoro wa shamba Mbarali waua wawili, watatu mbaroni kwa mauaji
Mbeya. Wakazi wa Igurusi wilayani Mbarali mkoani Mbeya, Wilbroad Mjengwa (38) na Maige Jirafu (44) wameauawa katika mgogoro wa kugombea shamba. Tayari Jeshi la Polisi mkoani hapa linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji hayo. Tukio hilo limedaiwa kufaywa na kundi la watu zaidi ya 15 ambapo mbali na kufanya mauaji hayo, pia walijeruhi wengine…