
Polisi wamsaka mganga anayedaiwa kusababisha kifo cha mwanafunzi
Arusha. Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara, limesema linaendelea kumsaka mganga wa kienyeji anayedaiwa kutoa ramli chonganishi iliyosababisha kifo cha mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Qash iliyopo wilayani Babati, mkoani Manyara, Yohana Konki (17). Yohana alifariki dunia baada ya kupigwa na wanafunzi wenzake kwa madai ya wizi wa kishkwambi, alfajiri ya…