
MENEJA TRA TEMEKE AONGOZA ELIMU YA KODI MLANGO KWA MLANGO TEMEKA NA KIGAMBONI
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza zoezi la elimu ya kodi mlango kwa mlango kwa wafanyabiashara wa Wilaya ya Kigamboni na Temeke mkoani Dar es salaam kwa lengo la kutoa elimu, kusikiliza changamoto na kuwakumbusha wafanyabiashara kufanya malipo ya awamu ya tatu kwa wakati. Zoezi hilo lililoanza Jumatatu wiki hii, limezinduliwa rasmi jana tarehe 09.09.2025…