
ACT Wazalendo yaibwaga CCM, ushindi watenguliwa
Kigoma. Mahakama ya Wilaya ya Kigoma imetengua ushindi wa Chama Cha Mapinduzi katika Mtaa wa Gezaulole, Kata ya Gungu, Manispaa ya Kigoma Ujiji, baada ya kujiridhisha kuwa haukuwa huru na wa haki. Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Katoki Mwakitalu, katika hukumu ya shauri la uchaguzi lililofunguliwa na mwanachama wa Chama cha Alliance for Change…