
Makonda ataka waliokula fedha za Tasaf waburuzwe kortini
Arusha. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Arusha, imesema inawashikilia watu watatu wakiwamo watumishi wa Mkoa wa Arusha kwa tuhuma za ubadhirifu wa Sh428 milioni. Fedha hizo zilitolewa kwa ajili ya utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf). Takukuru imesema inaendelea na taratibu ili kuwafikisha watuhumiwa hao mahakamani. Jana Jumamosi…