
SIRI IMEFICHUKA! Hiki hapa kinachoipa jeuri Yanga kususia ‘Dabi’
Jumatatu, Mei 5 mwaka huu, kamati ya utendaji ya Yanga ilitoa tamko zito la kugomea kucheza mechi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu dhidi ya mtani wao wa jadi Simba ‘Kariakoo Dabi’ ambayo awali ilikuwa ichezwe Machi 8 mwaka huu. Mchezo huo haukufanyika katika tarehe ya mwanzo baada ya kuahirishwa na Bodi ya Ligi…