
Maprofesa janga, wabunge wachambua hali halisi vyuo vikuu
Dodoma. Wabunge wametema nyongo kuhusu mustakabali wa elimu nchini, akiwamo mmoja aliyeonyesha wasiwasi wa ubora wa elimu, kwa vyuo vikuu kuwa na uhaba wa wahadhiri kwa ngazi ya uprofesa. Mbunge wa Viti Maalumu, Dk Tea Ntala amedai kwa sasa nchini kuna maprofesa 93, huku vyuo vilivyopo vikihitaji maprofesa 516. “Kwa sasa nchini tunao maprofesa 93…