
Ajali ya bajaji, Coaster yaua mama na mtoto
Mbeya. Mwanamke mmoja na mtoto wake ambao hawajafahamika majina wamefariki dunia baada ya ajali ya bajaji waliyokuwa wamepanda kugongana na basi aina ya Toyota Coaster Mtaa wa Maghorofani jijini Mbeya. Ajali hiyo ilitokea jana jioni, Mei 7, 2024 huku bajaji ikiwa imebeba watatu waliokuwa wanatokea hospitali ya mkoa. Imedaiwa kuwa, dereva wa bajaji hiyo aliyekuwa…