
Mashambulizi ya Lissu alianzia Kaskazini na Rais Samia, akaigeukia Kusini
Ndani ya wiki mbili zilizopita, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tanzania Bara, ametoa kauli mbili nzito. Mosi, mkoani Manyara, alitamka maneno yaliyotafsiriwa kama shambulizi kwa CCM na Rais Samia Suluhu Hassan. Ya pili, aliitoa Iringa, akikituhumu chama chake kwa rushwa. Manyara, Kaskazini ya Tanzania, Lissu alizungumza kauli tata kuhusu Muungano. Kwamba Samia Mzanzibari, asingekuwa Rais wa…