
Musoma Vijijini yatenga Sh280 milioni mradi wa nishati safi ya kupikia
Tarime. Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Vijijini mkoani Mara imetenga zaidi ya Sh280 milioni kwa ajili ya kutekeleza miradi ya nishati safi ya kupikia katika shule 22 za msingi na sekondari zilizopo ndani ya halmashauri hiyo. Bajeti hiyo inayotokana na mapato ya ndani, ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa…