
EU yatoa kauli barafu kilele cha Mlima Kilimanjaro
Moshi. Mabalozi 12 kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) wametembelea Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (Kinapa) na kueleza kuwa zinahitajika jitihada za makusudi kunusuru barafu ya Mlima Kilimanjaro, ambayo imeendelea kupungua kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Akizungumza katika lango la Marangu, jana Septemba 19, 2025 wakati wa kuhitimisha ziara ya siku…