
Trump ahukumiwa Marekani, hatokwenda gerezani
Washington. Hukumu ya kesi iliyokuwa ikimkabili Rais mteule wa Marekani, Donald Trump imesomwa leo na kumfanya kuwa Rais wa kwanza wa Marekani kuhukumiwa kwa makosa ya uhalifu. Pamoja na hukumu hiyo kutolewa leo Ijumaa Januari 10, 2025, Trump hatotumikia kifungo chochote wala kulipa faini katika shtaka la matumizi mabaya ya fedha kwa kumhonga mcheza picha…