
NJOMBE YAPOKEA MWENGE, LUDEWA YAANZA KUUKIMBIZA.
Mwenge wa Uhuru umepokelewa rasmi Mkoani Njombe katika Wilaya ya Ludewa ukitokea mkoani Ruvuma ambapo katika mkoa wa Njombe utakimbizwa Km. 726 na kupitia miradi yenye thani ya Tsh. Bil. 15.9. Wilaya ya Ludewa ndiyo Wilaya ya kwanza kuanza kuukimbiza mwenge huo katika mkoa wa Njombe ambapo itakimbiza umbali wa Km. 137 mpaka kukabidhiwa kwake…