
WAKAZI LOBO WATOA LAWAMA KWA VIONGOZI WA KIJIJI NA CCM KUKACHA MKUTANO WA DIWANI
-Wawatuhumu kuogopa kuulizwa uuzaji wa ardhi Na Mwandishi wetu, Simanjiro WAKAZI wa Kijiji cha Loiborsiret Wilayani Simanjiro mkoani Manyara, wamewashukia Mwenyekiti wa kijiji hicho Kimaai Saruni na Mwenyekiti wa CCM wa kata hiyo Aloyce Teme kwa kukacha mkutano wa Diwani wa kata ya Loiborsiret, Ezekiel Lesenga (Maridadi). Wananchi hao wamedai kuwa viongozi hao wamegoma kushiriki…