
Singida FG yajipata, Kyombo atakata Kirumba
Mwanza. Baada ya kuwa na matokeo mabaya kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa hatimaye leo wenyeji Singida Fountain Gate wamepata ushindi muhimu huku mshambuliaji wake, Habib Kyombo akitakata kwa kuifungia mabao mawili. Singida ambayo ilikuwa haijapata ushindi kwenye Ligi Kuu Bara tangu ilipoifunga Namungo bao 1-0 Machi 16, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM…