
Afariki dunia kwenye nyumba ya kulala wageni
Njombe. Erasto Raphaely (50), mkazi wa Kijiji cha Igelehedza kilichopo Kata ya Ilembula, Wilaya ya Wanging’ombe, amefariki dunia katika mazingira yanayotajwa kuwa ya kutatanisha akiwa ndani ya nyumba ya kulala wageni pamoja na mwanamke anayedaiwa kuwa mke wa mtu. Tukio hilo limetokea saa mbili usiku wa Jumapili ya Juni 8, 2025, ambapo marehemu aliripotiwa kuzidiwa…