
Mbwembwe zilivyomponza Dida, Azam ikiifuata Yanga nusu fainali FA
MBWEMBWE zilizoonyeshwa na kipa wa Namungo FC, Deogratius Munish ‘Dida’ zimeifanya timu hiyo kuruhusu bao la kizembe katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Azam kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi, usiku. Dida alionyesha mbembwe hizo katika dakika 17 ambapo alirudishiwa mpira lakini akajaribu kumtoka kwa kumpiga chenga Feisal Salum…