
Yanga yapokea ofa mbili za Mzize Ulaya
UONGOZI wa Klabu ya Yanga umethibitisha kupokea ofa kutoka katika timu za Ulaya ambazo zinataka kumnunua mshambuliaji Clement Mzize. Ingawa hakuwa tayari kuzitaja timu ambazo zinamtaka mchezaji huyo, lakini Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema mbali na Azam FC wamepokea ofa kutoka timu ambayo inashiriki Ligi Kuu Russia na nyingine ya Israel. “Ni kweli…