
AWAMU YA SITA YAIPIGA JEKI ELIMU ARUSHA – WALIMU WAPONGEZWA
Na Pamela Mollel,Arusha Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya maboresho makubwa katika sekta ya elimu mkoani Arusha kwa kutoa zaidi ya shilingi bilioni 267 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya elimu na ujenzi wa miundombinu ya shule. Akizungumza Septemba 17, 2025 kwenye Kongamano la Wadau wa Elimu…