Ujumbe wa Papa Francis kwa vijana wa kizazi kipya

Vatican. Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwapo maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia ya mawasiliano inayowawezesha watu wengi kuwasiliana. Hata hivyo, matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii yamekuwa chanzo cha kusambaratika kwa mawasiliano katika familia na jamii kwa ujumla. Padri Richard Mjigwa katika andiko lililochapishwa na mtandao wa Vatican News Aprili 28, 2025 amesema badala…

Read More

Wanafunzi wa Tanzania wang’ara shindano la Tehama China

Dar es Salaam.  Wanafunzi wa vyuo vikuu vya Tanzania na wakufunzi wameibuka washindi katika Shindano la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) linaloendeshwa na kampuni ya teknolojia nchini China, Huawei.  Fainali hizo za kimataifa kwa mwaka 2024/25 zilifanyika mjini Shenzhen, China huku wanafunzi kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikuu cha Dar…

Read More

Mgomo wa kufungua maduka wafika Mwanza, Mbeya

Dar/Mikoani. Wakati mgomo wa wafanyabiashara eneo la Kariakoo, Dar es Salaam ukiingia siku ya pili leo, umeungwa mkono na wengine wa mikoa ya Mbeya na Mwanza. Hata hivyo, katika maeneo hayo, baadhi ya wafanyabiashara wamefungua maduka na kuendelea na biashara kama kawaida. Kuendelea kufungwa kwa maduka katika eneo la Kariakoo, mbali ya kuwaathiri wateja, pia…

Read More

Polisi waimarisha ulinzi nje ya Kanisa la KKAM

Dar es Salaam. Lolote linaweza kutokea! ndiyo hali halisi iliyopo katika ibada ya Jumapili ya leo Julai 6, 2025 kwa waumini wa lililokuwa kanisa la ufufuo na uzima la Askofu Josephat Gwajima na wale wa Kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki (KKAM) dhidi ya Jeshi la Polisi. Waumini hao wameamua kufanya ibada ya pamoja tangu Jumapili…

Read More

Serikali yaagiza migodi ichungizwe kuepuka ajali

Shinyanga. Wakati shughuli za uokoaji zikiendelea kwenye mgodi wa Chapakazi wilayani Shinyanga ili kuwapata watu 18 walionasa ardhini, Naibu Waziri wa Madini, Dk Steven Kiruswa ameagiza kuchunguzwa migodi yote nchini ili kuepuka majanga. Ametoa agizo hilo leo Agosti 16, 2025 alipozungumza na wananchi eneo la ajali mgodini katika Kijiji cha Mwongozo, Kata ya Mwenge, wilayani…

Read More

Chaumma yashauri marekebisho Tume ya Uchaguzi

Mbeya. Pamoja na kuthibitisha kushiriki uchaguzi mkuu wa 2025, Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) kimependekeza na kuishauri Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) baadhi ya mambo ya kufanyiwa marekebisho kabla ya shughuli hiyo. Tanzania inatarajia kufanya uchaguzi mkuu Oktoba 25, 2025 kuwapata madiwani, wabunge na Rais huku chama hicho kikitarajia kusimamisha wagombea katika…

Read More

Askofu mstaafu Dk Mokiwa atoa ushahidi kesi ya ardhi

Dar es Salaam. Aliyekuwa Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk Valentino Mokiwa, ameieleza Mahakama Kuu, Divisheni ya Ardhi, jinsi alivyoshiriki mchakato wa kutoa eneo kwa ajili ya kupewa aliyekuwa Askofu wa kwanza wa dayosisi hiyo na Askofu Mkuu wa kanisa hilo, hayati John Sepeku. Hayati Sepeku alipewa na kanisa…

Read More