
Kimbunga Ialy kusababisha upepo mkali, mvua kubwa Jumanne
Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kimbunga Ialy kinachovuma kaskazini mwa kisiwa cha Madagscar, ambacho awali kilidaiwa kingeishia baharini, kinaendelea kupata nguvu na kinatarajiwa kusababisha mvua kubwa na upepo mkali Tanzania siku ya Jumanne Mei 21, 2024. Taarifa iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi leo Jumapili Mei 19,…