
Polisi wanne wa Intelijensia Moshi kortini wakidaiwa kutumia silaha kuiba bodaboda
Dar es Salaam. Askari wanne wa Kitengo cha Intelijensia cha Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Moshi, mkoani Kilimanjaro, wakikabiliwa na shtaka la wizi wa pikipiki ya abiria maarufu bodaboda kwa kutumia silaha. Maofisa hao wa Polisi, wanatuhumiwa kuiba pikipiki hiyo mali ya Ramadhani Singe katika kambi ya Polisi….