Wakazi wa Malinyi waiomba Serikali kuboresha miundombinu ya barabara ili kufikia masoko ya mazao yao

Farida Mangube, Morogoro . Wakazi wa Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro wameiomba serikali kuboresha miundombinu ya barabara ikiwemo madaraja ili kuwawezesha kufikia masoko kwa urahisi na kuuza mazao yao kwa bei ya soko. Wakazi hao, ambao wengi wao ni wakulima wa mazao ya biashara na chakula wanasema kukosekana kwa barabara za uhakika kumeendelea kuwafanya wategemee…

Read More

Sudan imenaswa katika 'jinamizi la ghasia', mkuu wa Umoja wa Mataifa ameliambia Baraza la Usalama – Global Issues

“Mateso yanaongezeka siku hadi siku, na karibu watu milioni 25 sasa wanahitaji msaada wa kibinadamu,” Bwana Guterres. aliiambia mabalozi katika Baraza la Usalamaakisisitiza hali mbaya ambayo raia wanavumilia Miezi 18 kwenye mzozo. Alitaja hali hiyo kuwa ni mfululizo wa ndoto mbaya zisizoisha. “Maelfu ya raia waliuawa, na wengine isitoshe wakikabiliwa na ukatili usioelezekakutia ndani ubakaji…

Read More

NRA kuunda Serikali yenye Wizara 10 ikishinda uchaguzi

Mirerani. Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), Almas Kisabya amesema endapo atachaguliwa kuwa Rais, ataunda Serikali ndogo yenye wizara zisizozidi 10, lengo likiwa kufanikisha utendaji kazi. Kisabya ameyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni ya urais leo Ijumaa Septemba 12 mwaka 2025 mjini Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara. Amesema endapo atachaguliwa…

Read More

Fisi aliyekutwa amekufa akiwa na jina, shanga azua gumzo

Itilima. Fisi mmoja ameuawa katika Kijiji cha Kimali kilichopo katika Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu na kukutwa akiwa amevalishwa shanga shingoni na alama ya jina kwenye paja lake la mguu wa kushoto, jambo ambalo limezua gumzo katika mkoa huo. Tukio hilo la kushangaza limeweza kuibua maswali mengi kuhusu asili yake kama alikuwa na mmiliki au alikuwa sehemu…

Read More

CEO NMB awafunda Wahitimu ‘Form Four’ Charlotte Sekondari

NA MWANDISHI WETU, MOROGORO KUELEKEA mitihani ya Taifa ya Kidato cha Nne itakayofanyika Novemba 11, 2024, wahitimu wa Shule ya Sekondari Charlotte iliyopo Tungi Mkwajuni, Manispaa ya Morogoro, wametakiwa kumtanguliza Mungu, kuwa na nidhamu, bidii, uadilifu na uaminifu, ili kupata mafanikio zaidi kielimu, kimaisha na kiimani. Wito huo umeetolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki…

Read More

Machungu ya vivuko boti zikitumika, nane zakamatwa

Dar es Salaam. Makali ya upungufu wa vivuko kati ya Magogoni na Kivukoni yanaendelea kuwatesa wananchi ambao licha ya kuonywa na mamlaka, wameendelea kuvushwa na boti zinazohatarisha usalama wao.  Taarifa ya Kikosi cha Polisi Wanamaji iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana, inathibitisha adha wanayopitia wananchi hao kutokana na kutofanya kazi kwa vivuko vya Mv Magogoni…

Read More

Ni zamu ya Ali Maua Kijitonyama

Leo imekua zamu ya Ali Maua Kijitonyama kufikiwa na kampuni ya Meridianbet ambapo wameendelea kufanya ambayo wamekua wakiyafanya mara kwa mara ambapo wamefanikiwa kutoa msaada kwa jamii. Meridianbet wamefanikiwa kufika eneo la Kijitonyama Ali Maua leo na kutoa msaada kwafamilia mbalimbali ambazo zinapitia changamoto mbalimbali na zisizojiweza, Hii inaendeleakuonesha namna mabingwa hao wa kubashiri wanavyoijali…

Read More