
Miili 36 ya ajali ya Same ilivyoagwa KCMC
Moshi. Ni siku iliyojaa huzuni na majonzi wakati familia za watu 36 kati ya 42 zikiaga miili ya wapendwa wao waliofariki dunia katika ajali ya magari mawili ya abiria wilayani Same, mkoani Kilimanjaro. Shughuli ya kuaga miili hiyo imefanyika leo Alhamisi Julai 3, 2025 kwenye viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC)…