Simbu amaliza wa pili mbio za Kolkata India
MWANARIADHA maarufu nchini, Alphonce Simbu, ameendelea kuonyesha kiwango cha juu kimataifa baada ya kumaliza nafasi ya pili katika mbio za Kolkata zilizofanyika leo Jumapili huko India. Katika mbio hizo za kilomita 25, Simbu alitumia saa 1:11:56 kumaliza wa pili nyuma ya Joshua Cheptegei wa Uganda aliyeshinda kwa saa 1:11:49, huku ushindani ukiwa mkali kati ya…