
Josiah: Mashujaa tuko nao, kipa mzuka mwingi
WAKATI Tanzania Prisons ikiendelea kujifua kwa ajili ya mwendelezo wa Ligi Kuu Bara, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Aman Josiah amesema kikosi chake kipo tayari na Mashujaa wajiandae kisaikolojia kuacha pointi tatu. Prisons inatarajia kushuka uwanjani Februari 6, kuikaribisha Mashujaa kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya ukiwa ni wa mzunguko wa pili wa ligi hiyo…