
Bunifu 42 za Kitanzania tayari kwenda sokoni
Dodoma. Bunifu na teknolojia 42 kati 283, zilizoibuliwa kupitia Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (Makisatu) na kuendelezwa kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), zimefikia hatua ya kuingia sokoni. Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga amesema hayo leo Jumanne Aprili 30, 2024 alipokuwa akijibu swali la msingi…