
Rais Ruto aitisha kikao cha baraza la mawaziri kuhusu mafuriko makubwa yalioikumba Kenya
Rais wa Kenya William Ruto aliitisha kikao maalum cha baraza la mawaziri siku ya Jumanne kujadili hatua za kukabiliana na mafuriko ambayo yamesababisha vifo vya karibu watu 170 na wengine 185,000 kuyahama makazi yao tangu Machi, ofisi yake ilisema. Mvua kubwa kuliko kawaida za masika, zikichangiwa na hali ya hewa ya El Nino, zimeharibu nchi…