
Hamas na Fatah wazungumza na kulenga kufikia maridhiano – DW – 30.04.2024
Makundi hasimu ya wapiganaji wa Kipalestina ya Hamas na Fatah wameeleza nia yao ya kisiasa ya kutaka maridhiano kwa njia ya mazungumzo walipokutana mjini Beijing. Hayo yameelezwa hii leo na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China Lin Jian: “Kutokana na mwaliko wa China, wawakilishi wa kundi la Fatah na Hamas waliwasili Beijing hivi karibuni…