
Nondo wa ACT-Wazalendo adaiwa kutekwa, Polisi yasema…
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT-Wazalendo, Abdul Nondo anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana katika Kituo cha Mabasi cha Magufuli kilichopo Mbezi Luis wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam. Nondo anadaiwa kukutwa na kadhia hiyo leo Jumapili Desemba mosi, 2024 muda mfupi baada ya kushuka katika basi akitokea mkoani Kigoma alikokuwa akishiriki…