Ndege ya jeshi yaanguka shuleni yaua wanafunzi 16

Bangladesh. Watu 19 wamefariki dunia nchini Bangladesh baada ya ndege ya jeshi kamandi ya anga kuanguka katika eneo la Shule na chuo cha Milestone jijini Dhaka, leo Jumatatu Julai 21, 2025. Ndege hiyo ya mafunzo ya kijeshi kwa mujibu wa Al Jazeera imeanguka saa saba mchana wa leo wakati wanafunzi wa shule hiyo iliyopo mtaa…

Read More

Walimu wadaiwa kuiba maharage, mahindi ya shule Makambako

Njombe. Wazazi wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Magegele Kata ya Kivavi Halmashauri ya Mji wa Makambako mkoani Njombe, wameitaka halmashauri kuwachukulia hatua za kisheria walimu ambao wamebainika kujihusisha na wizi wa mahindi na maharage ya shule. Wamesema vinginevyo hawatakuwa tayari kutoa tena mchango wa chakula shuleni hapo. Kauli hiyo wameitoa leo Julai 14, 2025…

Read More

Heche: Tupo tayari kwa hatua ngumu kuelekea uchaguzi mkuu

Tarime/Dar. Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, John Heche amesema chama hicho kipo tayari kutembea katika hatua ngumu inayotarajiwa kufikiwa baada ya kukamilisha utoaji elimu kuhusu msimamo wa bila mabadiliko hakutakuwa na uchaguzi. Katika kauli yake hiyo, Heche amesema kwa sasa chama hicho kinalenga kuwafikia viongozi wa dini, balozi za mataifa mbalimbali ili kuzielimisha kuhusu msimamo…

Read More

Madaktari wanane wanatibu wagonjwa 10,000 Tanzania

Dodoma. Wakati Shirika la Afya Duniani WHO likiweka uwiano wa madaktari 22.8 kutibu watu 10,000 kwa nchi zinazoendelea, Tanzania imebainika kuwa na uwiano wa madaktari 8.4 wanaotibu watu 10,000 sawa na theluthi moja. Hayo yamesemwa leo Januari 28, 2025 na Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Stanslaus Nyongo kwa niaba ya Waziri…

Read More

Samia atoa mwelekeo mpya Zanzibar

Unguja. Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuzilinda tunu za Muungano, amani na utulivu wa Taifa kama walivyoziacha waasisi, Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume, kwa ajili ya vizazi vijavyo. Pia, ameahidi kujenga kituo cha kumbukumbu na nyaraka za Muungano ili wageni wanaoitembelea…

Read More

RPC Mkama ataka wananchi kutunza miondombinu reli SGR

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama amekaa kikao na Polisi Kata wanao zihudumia Kata zilizopitiwa na mradi wa treni ya mwendokasi (SGR) na kupanga Mikakati ya Ulinzi wa miundombinu ya reli hiyo. Akiongea na Polisi Kata hao wenye vyeo vya Wakaguzi na Wakaguzi Wasaidizi ,Rpc Mkama amesema, Morogoro imepitiwa kwa kiasi kikubwa…

Read More

Hamdi awataja Chama, Pacome | Mwanaspoti

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miloud Hamdi, kwa sasa ameanza hesabu kwa ajili ya Dabi ya Kariakoo, huku akiwataja viungo washambuliaji wa timu hiyo ambao wameifanya Yanga kuwa imara hadi sasa licha ya kuondokewa na Stephane Aziz KI aliyepo Wydad Casablanca ya Morocco. Kocha huyo aliyetua katikati ya msimu akitokea Singida Black Stars ili kuchukua nafasi…

Read More