
Kikokotoo chaendelea kufukuta, Tucta, THTU wakoleza moto
Dodoma. Baada ya malalamiko ya wafanyakazi kuhusu kanuni mpya za kikokotoo cha mafao ya mkupuo, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) limesema limewasilisha maoni kwa Serikali na bado majadiliano yanaendelea. Kanuni mpya za mafao ya mkupuo zilianza kutumia Julai 2022 ambapo mafao hayo kwa mifuko yote ya hifadhi ya jamii ni asilimia 33. Tucta…