TBS YATOA ELIMU KWA WAJASIRIMALI KWENYE MAONESHO YA MUUNGANO

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetoa elimu ya viwango vya ubora kwa Wajasiriamali wadogo waliojitikeza katika Maonesho ya Kibiashara ya Miaka 60 ya Muungano katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo leo Aprili 25,2024, Afisa Masoko (TBS), Bw. Mussa Luhombero amesema wametoa elimu…

Read More

Mbowe akatisha mkutano wake Geita kisa mvua

Geita. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa hatima ya maisha ya Watanzania ipo kwenye mikono, mioyo na akili zao. Amesema kila kona ya nchi kuna malalamiko bila kujali aina ya shughuli wanazofanya na kusema, utafiti uliofanywa na chama hicho umebaini malalamiko na matatizo mengi ya wananchi yanatokana na mfumo wa utawala unaotokana na Katiba…

Read More

BUNGE LAPITISHA SH. TRILIONI 1.8 MATUMIZI YA WIZARA YA NISHATI 2024/2025

-95.28% kuelekezwa kwenye maendeleo-Serikali kuja na Kanuni ya Uwajibikaji kwa wananchi Miradi ya Mafuta na Gesi Asilia-Dkt. Biteko aagiza Halmashauri kupeleka fedha za Ushuru wa Huduma vijijini-Masharti ufunguzi wa vituo vya CNG yarekebishwa kuvutia uwekezaji-Kapinga atilia mkazo utekelezaji Nishati Safi ya Kupikia na CNG Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limepitisha shilingi Trilioni…

Read More

Mvua ya maafa yazidi kutikisa nchini

Dar/mikoani. Ni wimbi la majanga lililopoka uhai wa binadamu, kuathiri makazi na hata kukwaza shughuli za kiuchumi, ndiyo lugha nyepesi unayoweza kuitumia kuakisi kiwango cha athari za mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini. Mvua hizo za El-Nino zilizoanza kunyesha Oktoba mwaka jana, hadi sasa zimefululiza kwa miezi saba na kukatisha uhai wa watu  162 nchini,…

Read More

PPRA, ZPPDA zasaini makubaliano kuenzi miaka 60 ya Muungano

Na Mwandishi Wetu Wakati kesho Tanzania ikisherehekea miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) na Mamlaka ya Ununuzi na Uondoaji wa Mali za Umma Zanzibar (ZPPDA) zimesaini rasimu ya mkataba wa maelewano (MOU) kufanya kazi pamoja na kuimarisha muungano. Makubaliano hayo yamesainiwa leo jijini Dodoma mbele…

Read More

Rais Samia akabidhi Muungano kwa vijana nchini

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amesema uimara na uendelevu wa Muungano uko mikononi mwa vijana. Kutokana na hilo, amesema: “Ninawasihi sana vijana wote wa Tanzania muwe walinzi wa Muungano wetu. Kumbukeni kuwa Muungano huu ni urithi na tunu ya Taifa letu, na ni tunu ya Afrika kwa ujumla.” Samia amesema hayo jana alipohutubia…

Read More