
Ahoua aibeba Simba ikijiimarisha kileleni
SIMBA imeokota pointi tatu zingine ngumu kwenye mchezo uliotoa mshindi dakika za jioni ikiichapa JKT Tanzania kwa bao 1-0, ushindi ukiendelea kuwaweka kileleni katika sikukuu ya Krismasi inayoadhimishwa kesho Jumatano Desemba 25. Bao la kiungo mshambuliaji Jean Charles Ahoua aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Awesu Awesu akilifunga dakika ya 90+5 kwa mkwaju wa penalti baada…