
Clara Luvanga namba zimempa heshima Saudia
KAMA kuna msimu bora kwa mshambuliaji wa Kitanzania, Clara Luvanga anayeitumikia Al Nassr ya Saudia basi ni huu. Mambo ambayo ameyafanya msimu huu hasa kuwatesa mabeki na makipa wa timu pinzani kwa mabao ya mbali yamempa sifa kubwa nyota huyo wa Kitanzania. Sio jambo la ajabu kumuona nyota huyo akionyesha kiwango bora kwani amekuwa akifanya…