Mzungu aliposhindwa kutamka songela akaita Songea
Songea ndio mji unaoubeba Mkoa wa Ruvuma ambao kabla ya uhuru ulikuwa sehemu ya jimbo la kusini sambamba na Mtwara na Lindi. Kwa mujibu wa Chifu wa Wangoni, Imanuel Zulu, jina Songea lilitokana na neno songela linalomaanisha mlango na kwamba mtawala wa kwanza wa Wangoni Chifu Inkosi Mputa bin Gwazerapasi Gama, aliwafungulia watu mlango kuingia…